JINSI YA KUPATA MTAJI NA KUANZISHA DUKA LAKO LA DAWA/VIPODOZI/FAMASI
0788179686 | afyazaidi@gmail.com | https://afyazaidi.co.tz
Napenda kuona watu wanafanikiwa kuanza biashara zao. Napenda kuona watu wanakuza mtaji na kukuza biashara zao. Ila Mtaji bado unabaki changamoto sana kwa watu waliowengi kiasi cha kushindwa kabisa kuanza biashara au kufanikiwa kuanza lakini kushindwa kukua na kuweka biashara zao katika muonekano mzuri.
Mimi mwenyewe naelewa vizuri tatizo hili la mtaji personally maana kuna kipindi katika maisha yangu nilitamani sana kufanya mambo makubwa lakini nilishindwa kwa sababu mtaji ulikuwa hautoshi. Nilipomaliza chuo nilitamani sana kuwa na kiwanda changu cha dawa na nifanye uzalishaji wa dawa humu humu nchini. Ila kucheki mahitaji yake ya mtaji daaaahhhh nikajua hili sio fungu langu bora niangalie vitu vingine kwanza. Billioni moja (Tsh 1,000,000,000) na zaidi mimi natoa wapi??? Haa haa haaaa……..
So tukija kwenye hizi biashara ambazo nawahamasisha kila siku kama maduka ya vipodozi, maduka ya dawa muhimu (DLDM), famasi na kadhalika kwenyewe ni simple tu; kwa mfano Tsh Millioni 5 hadi Millioni 8 unafungua duka la vipodozi safi tu; au duka la dawa muhimu (DLDM) la kiwango kizuri cha ubora. Tsh Millioni 20 hadi Tsh Millioni 25 unafungua famasi nzuri tu na kutimiza ndoto yako ya kufanya biashara hiyo. Ila ishu inakuja kwamba kuna nyakati hata hiyo Millioni 5 inayoonekana ndogo inakupiga chenga; achilia mbali hiyo millioni 20 - 25.
Ukiwa kwenye wakati kama huo ufanyeje ili uweze kupata mtaji na kuanza biashara yako?
Kwa bahati nzuri kuna njia. Na moja au zaidi ya hizi njia ikifanikiwa basi utapata mtaji na kuanza au kuboresha biashara yako. Cha msingi kuwa makini na uchague njia ambayo inaendana na mazingira yako. Vinginevyo unaweza kujiingiza katika matatizo makubwa kuliko hata lile la mwanzo la kukosa mtaji.
Tumia moja au baadhi ya njia zifuatazo ili kuweza kupata mtaji na kuanza biashara yako:
Weka pembeni kiasi fulani cha pesa kila mwezi na iache hiyo pesa ikue bila kuidokoadokoa hadi malengo yako yatimie. Mfano kama unalipwa mshahara Tsh 800,000 kwa mwezi (Take home) basi unaweza kuweka Tsh100,000 kila mwezi na hivyo kuweza kuwa na Tsh 1,200,000 kwa mwaka; fanya hivyo pamoja na vyanzo vingine na baada ya muda utajikuta una kiasi kizuri tu cha pesa kwa ajili ya biashara yako.
Jiunge na Saccos au Vicoba, weka akiba kila mwezi kisha baada ya muda chukua mkopo. Ni hatari kuchukua mkopo na kuanzisha biashara, ila haya maisha sometimes bila kujilipua hutoboi ng’o!
Anza biashara ndogo kwa lengo la kukuza mtaji kisha iuze au ibadili kuwa biashara yako kubwa. Kama una Tsh 5,000,000 anza na duka la dawa muhimu sehemu yenye biashara nzuri. Baada ya miaka 3 hadi 5 mtaji wako utakuwa umekua hata zaidi ya Tsh 22,000,000 + network + uzoefu na hivyo kukuwezesha kufungua biashara yako pendwa - Famasi.
Kusanya nguvu na wenzako mufanye biashara pamoja. Kama wewe una Tsh 1,000,000 ukipata wenzako wanne wenye Millioni Moja kama wewe jumla munakuwa na Tsh 5,000,000 kisha munaanza biashara yenu ya vipodozi mdogomdogo kwa mtaji wa shillingi Millioni 5! Ila kuwa makini sana na njia hii, waswahili hatuwezi kufanya pamoja biashara kwa muda mrefu. So mjisajili mapema kisheria ili huko mbele ya safari wengine wakigeuka basi haki za wengine zisipotee
Kama una dhamana basi kachukue mkopo benki. Ni rahisi na haraka zaidi, ila njia hii majuto ni mjukuu.Mara nyingi inakuja kuwa kwamba muda wa kuanza kufanya marejesho ushafika ila wewe biashara yako bado haijasimama vizuri hivyo unayumba kifedha na hata kushindwa kurejesha mkopo vizuri.
Fanya kazi za ziada ili kuongeza kipato chako na weka akiba kubwa zaidi. Hii njia naipenda sana. Yaani kwa mfano wewe ni muhasibu unafanya kazi katika kiwanda cha saruji basi bado unaweza kusaidia kampuni ndogo ndogo ambazo hazina muhasibu wao waliyemuajiri - migahawa, hoteli, famasi na kadhalika katika shughuli zao kisha wakawa wanakupoza let say Tsh 200,000 hadi Tsh 500,000 kwa mwezi kutegemea na ukubwa wa biashara na kazi zenyewe. Unaweza kujiongeza na kusaidia maeneo 2 hadi 3 kwa mwezi na hivyo kulaza Tsh 600,000 hadi Tsh 1,500,000! Utafanya nini na huu “mpunga” wako mpya??? Hii ipo kwa fani mbalimbali sio kwa wahasibu au sekta rasmi tu; unaweza kuwa daktari na ukafanya part time sehemu baada ya kutoka hospitali kwako ulikoajiriwa; au ukawa unafanya kazi ya kufundisha chuo baada ya kutoka huko kazini kwako.
Njia ni nyingi naweza kuandika na kuongea hadi kesho. Naomba feedback yako - kati ya njia hizo hapo ipi umeiona au zipi umeziona kwako zinaweza kukusaidia kuanzia? Tafadhali niambie nijue kama andiko langu limekusaidia lolote. Natanguliza shukrani - Ahsante!
Kwa ushauri zaidi usisite kucheki nasi AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS na tutakusaidia kupunguza risk na kuongeza chance ya kufanikiwa kwa wakati. 0788179686 | afyazaidi@gmail.com | https://afyazaidi.co.tz.
Bye!
Ofcoz kutoboa inaitaji moyo daa kweli milion 5 unakuta ni kisima kilefu kuipata
Nina mtaji wa milioni 1 ndoto yangu nikufanya biashara ya vipodozi nifanyeje ilikuweza kufikia malengoo ?