UPO TAYARI KUANZA BIASHARA YAKO?
Njoo Tukusaidie Kupanga Bajeti, Kupata Vibali, Kupata Bidhaa Za Kuanzia Na Wateja Wa Kufaulisha Biashara Yako
Wafanyabiashara waliokwama na famasi zao, maduka yao ya dawa muhimu, maduka yao ya vipodozi, dispensary, hospitali, maabara na kadhalika hutuita tuende tukaangalie tatizo ni nini, wamekwama wapi na nini wafanye ili kujikwamua na kuendelea vizuri na biashara.
Baadhi ya matatizo ambayo tumeyakuta sehemu nyingi ni bei kubwa ukilinganisha na wenzake walio eneo karibu yake, kuchelewa kufungua, kuwahi kufunga, kutokuwa na wateja wengi wanaosupport duka lake, kukosa bidhaa ambayo wateja wanaitaka na kadhalika.
Mengi kati ya hayo matatizo hutokana na kutokujipanga vizuri. Yaani usimamizi mbaya. Kutojua kwa wakati ni nini kitatakiwa na kukiweka tayari. Kutotimiza mahitaji ya wateja na hatimaye wanaenda kutafuta mahitaji yao sehemu zingine. Kutokuwa na sifa ambazo wateja watakuwa wanaliongelea duka au kituo na kwenda kutangaziana. Kutovutia wateja wapya. Na kadhalika.
So sisi #afyazaidiconsultants kama washauri huwa tunafanya tathmini ya hali ya sasa ya biashara, matatizo gani yapo, namna inavyotakiwa kuwa, vitu gani vimekosekana, vitu gani vifanyike ili kutatua matatizo hayo na kufika pale ambapo biashara inatakiwa ifike na kisha kumsaidia mwenye biashara yake katika utekelezaji hadi atakapofanikiwa kujinasua.
Wafanyabiashara wengi wanafurahi sana baada ya kupata suluhisho la matatizo ya biashara zao. Wanafurahi kufanya kazi na sisi.
Na sisi tunafurahi sana kuweza kutatua matatizo mbalimbali ya biashara hizo na kutimiza mahitaji yao. Ndio kazi yetu, ndio maisha yetu.
Nawe pia kama umekwama au ndo unataka kuanza basi tucheki ufurahie safari yako .......
#afyazaidiconsultants
#afyazaidi
#afyazaidiadvisor
#pharmacy
#dukalavipodozi
#hospitali
#dukaladawa