Kabla ya kujiumiza kupunguza uzito wako fikiria mambo mawili:
Uzito wako unaongezekaje?
Maisha gani yanakusababisha kuongezeka uzito?
Aghalabu uzito huongezeka kutokana na vyakula hususan jamii ya wanga (wali, ugali, viazi, ndizi, chapati, maandazi, tambi, mikate na kadhalika) na mafuta. Mwili wako una mahitaji mahususi ya vyakula aina zote kwa ajili ya kujijenga, kuzalisha nguvu, kufanya kazi vizuri, kujikinga dhidi ya magonjwa na kuendelea. Ukila kiasi kama kinachohitajika na mwili wako basi chakula chote kitatumika na wewe hautabaki na akiba mwilini, hautaongezeka uzito wala unene kupitiliza. Ukila kiasi zaidi ya kinachohitajika na mwili wako basi kuna kiasi hakitatumika na kitahifadhiwa kama akiba mwilini, kitakuongezea uzito na kukunenepesha.
Ukiushughulisha sana mwili wako kwa kazi za nguvu na mazoezi basi matumizi yako ya chakula mwilini yataongezeka na akiba iliyojijenga mwanzo itatumika, hatimaye kukupunguzia uzito na unene.
SASA ANGALIA MAISHA YAKO
a) Unakula sana vyakula vya aina gani?
Maana vyakula vya wanga na mafuta vinaongeza uzito wako, na vyakula jamii ya protini (Samaki, nyama, maziwa, maini, mayai, kuku, maharage na kadhalika) na mboga za majani haviongezi sana uzito wako.
b) Unajishughulisha na kazi gani za kutumia nguvu?
Unanyanyua mizigo mizito, unakimbia, unatembea sana, unafanya sana mazoezi ya viungo, unaogelea sana au vipi?
Afya Zaidi Tip: Njia nzuri isiyo na gharama ya kudhibiti uzito wako ni kula kulingana na mahitaji ya mwili wako na kuushughulisha mwili wako ili kuzuia chakula kubaki na kuhifadhiwa mwilini.
Ukiweza kujidhibiti kutokula zaidi ya mahitaji yako na kuushughulisha mwili wako kwa mazoezi na kazi za nguvu basi utaweza kabisa kudhibiti uzito wako usiongezeke.
UFANYEJE ILI KUPUNGUZA UZITO WAKO?
Ni rahisi. Acha au punguza kabisa kula vyakula vya wanga na mafuta; ongezea na mazoezi makali na kazi nyingi za kutumia nguvu. Mwili wako utalazimika kuunguza akiba ya chakula kilichopo mwilini mwako ili kuongezea nguvu, akiba ya chakula itapungua na hatimaye uzito wako utapungua na wewe utapungua unene. Hadi hapo najua hakuna siri wala porojo, ni rahisi tu na ni wazi kabisa.
Ila jiulize, sasa kama ni rahisi hivi je kwa nini watu wengi wanashindwa?
So far Afya Zaidi (AZ) Consultants tutakupa jibu moja zuri: Watu wanaoshindwa wanajua tu nini cha kufanya, ila hawajui jinsi ya kufanya vizuri na hawafanyi vizuri; yaani hawana mpango mkakati mzuri na utekelezaji wao sio makini. Mtu anatamani kupungua kilo 10 ndani ya mwezi mmoja, mazoezi anafanya mara 2 hadi 3 kwa wiki na ni ya kivivuvivu; kisha anakula ugali, wali, chipsi na kadhalika kama kawaida. Na hana mtu wa kumuongoza, kumsimamia wala kumtia hamasa au kumsisitiza. Mtu huyu hawezi kufanikiwa. Wengine nimeona wanapenda short-cut kwa kutumia dawa tu ili uzito upungue huku wao wakiendelea na mtindo wao wa maisha kama kawaida.
Ndo hivyo tu. Kwa hiyo ni matokeo ya mpango mbaya na utekelezaji mbovu.
Sasa kama wewe unataka kupunguza uzito wako basi weka mpango madhubuti na kuwa na utekelezaji mzuri. Na sisi Afya Zaidi (AZ) Cosnultants tutakusaidia kutimiza malengo yako. Utapungua kilo 5, 10, 15, 20, 30, 40 na kuendelea.
Ingiza email address yako na bonyeza button ya “Subscribe now” hapo chini ili kujifunza zaidi kutoka kwetu na kuweza kutatua kero mbalimbali zinazokukabili na kufanikiwa katika kuanzisha na kusimamia vizuri biashara yako pendwa. Ni Bure!
MWAMBIE NA MWENZIO ……