Bado nashangaa kwa nini watu wengi walioamua kupunguza uzito wanakwama kupungua na hatimaye wanakata tamaa wanaacha wanaendelea kunenepa na kuongezeka uzito.
Kwa nini? Changamoto kubwa haswa huwa ni nini?
Maana ukitaka kupunguza uzito wako ishu kubwa ni kupunguza kula vyakula vinavyoongeza uzito na kuzidi kufanya shughuli zinazotumia akiba ya chakula mwilini, mfano mazoezi ya kukimbia na kuruka kamba.
Unapunguza kula vyakula vyote vyenye wanga/sukari kama vile maandazi, chapati, pizza, burger, mikate, ugali, wali, tambi, ndizi, mananasi, embe nk na badala yake unakula zaidi samaki, nyama, maini, mayai, mtindi, korosho, karanga nk.
Kimbia, ruka kamba, ruka kichurachura nk angalau nusu saa kila siku na utaona matokeo mazuri.
Tazama, kama unataka kufanikiwa shika mambo mawili tu ya kuanzia:
1. Mpangomkakati
2. Nidhamu
Lengo lako ni kupunguza uzito wako. Panga kabisa unataka kupunguza kilo ngapi ndani ya muda gani (LENGO). Kisha ainisha ni mambo gani utafanya, kiasi gani utafanya na muda gani utafanya ili kuimiza lengo lako (MPANGO). Malizia kwa kujidhatiti ni jinsi gani utafanya hatua kwa hatua hayo mambo ili kutekeleza mpango wako (MKAKATI).
Ukishakuwa na mpangomkakati mzuri na kuutekeleza vizuri kabisa basi kupungua uzito ni jambo la uhakika na hautaamini jinsi ilivyo rahisi.
Ni mimi mwalimu wa diet, AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS!
0788179686 | afyazaidi@gmail.com