Watu wetu wengi mnafikiria mambo makubwa sana na mazuri. Yaani ingekuwa kila mnachowaza kinakuwa basi hapa Tanzania kungekuwa na biashara kubwa nyingi sana zinazomilikiwa na watu wa aina mbalimbali - wanawake, wanaume, wazee, vijana, waajiriwa, wanafunzi wa chuo, wasomi wa kubwa, wasiosoma sana nk.
Akili na mawazo mazuri ni mengi sana. Ukiyasikia kutoka kwa mtu aliyekwama sehemu anaomba ushauri unaona kabisa ebwana eeehhhhh hili ni bonge la idea litakalokuja kutatua tatizo kubwa na kufanikisha mahitaji ya watu wengi.
Watu Wana idea za viwanda, kampuni za software muhimu, vyuo, mashamba makubwa ya kisasa, kusaidia wajasiriamali kupata mitaji kwa gharama nafuu, kutibu magonjwa, ujenzi wa gharama nafuu nk.
Tumekwama wapi?
1. Ni kutoka 0 kwenda 1.
Hapa ni pagumu sana, hususan kwa kitu ambacho ndio unaanza mara ya kwanza. Mfano mtu mwenye mabasi 10. Huyu basi ambalo lilimtesa sana kununua na kukaa sawa kibiashara ni lile la kwanza. Kadhalika na mtu mwenye Famasi 5, au yule mwenye nyumba 5, kampuni 3, pikipiki 10 au saluni 7. Ndio maana unaambiwa ukitaka urahisi basi fungua tena biashara nyingine kama ile ambayo umefanikiwa na una uzoefu nayo tayari. Yaani ukifanikisha basi moja wewe nunua basi jingine, na jingine na kisha jingine. Ni rahisi zaidi kuliko kuanza kitu cha tofauti kabisa kama kufungua Famasi au saluni au kilimo.
2. Ukifanikisha kufika 1 na kukaa vizuri kibiashara changamoto inayofuata ni kusonga kutoka 1 na kwenda 2; kisha kutoka 2 kwenda 3; 3 kwenda 4; na kadhalika.
Hapo ndipo ndoto nyingi zinaishia kuwa ndoto tu. Tunashindwa kuanza, kukaa sawa na kusonga mbele zaidi. Sababu huweza kuwa kukosa taarifa za kutosha (Data), mpango mzuri, mkakati mzuri, rasilimali za kutosha na hata soko kubadilika.
Tupambane jamani. Tuongeze nguvu na akili. Tuone tunapoenda, tujue jinsi ya kufika na tuende vizuri kabisa kwa mahesabu na imani.
Sisi AFYA Zaidi (AZ) Consultants tutaendelea kuwasaidieni wapambanaji wote taarifa za kutosha, maono mazuri, njia, mipango na mikakati mizuri, kutatua matatizo, kuondoa vikwazo na kufikia malengo.
Twende Pamoja. Pata ushauri upige hatua: https://azc.co.tz/contact-us
#azalo