UKITAKA KUFANIKIWA ANZA NA USIMAMIZI MZURI
USIMAMIZI MBOVU UNAWEZA KUZOROTESHA AU KUFELISHA KABISA BIASHARA YAKO
Ukitaka kufanikiwa katika biashara yako hususan inayohusiana na afya basi hakikisha unakuwa na usimamizi (management) nzuri sana ili usisumbuliwe na matatizo, usiyumbe au biashara yako isife. Usimamizi (Management) ndio kila kitu - kukidhi vigezo na masharti ya kutoa huduma, kuwa na bidhaa na huduma nzuri, kuvutia wateja, kuwa na mauzo mazuri, kubaki na faida nzuri, mtaji kukua, wafanyakazi kufanya kazi vizuri, kuwa na amani na utulivu katika biashara yako, kuendelea, kukua, kupata usaidizi kwa haraka kila ukihitaji na kadhalika.
Ukiwa na usimamizi mbovu tu basi matatizo mengi yatajitokeza ambayo ukishindwa kukabiliana nayo basi biashara yako itayumba na hata kufa - Malalamiko ya wateja yatakuwa mengi na makubwa, mauzo yatapungua, mtaji utapungua au kuisha kabisa, madeni, kesi, wafanyakazi kuacha kazi na kuondoka, upotevu wa pesa na vitu, migogoro kazini, matatizo na serikali, faini, kusimamishwa au kufungiwa kabisa na serikali, mashine na vifaa kuharibika mara kwa mara, kutokuwa na huduma za kutosha, kutokuwa na bidhaa za kutosha na kadhalika.
Cha msingi kwako wewe kama mfanyabiashara au mwekezaji ni kuwa na usimamizi (management) nzuri na washauri au wakaguzi wa usimamizi (management) wako ili kuhakikisha kwamba mara zote uko vizuri na kila kitu kinaenda sawa.
Kama una tatizo katika eneo la biashara yako na unahitaji msaada basi wasiliana nasi tutakusaidia kulitatua.
#Usimamizi
#Management
#afyazaidiconsultants
#afyazaidishop
#afyazaidiadvisor