SABUNI YENYE DAWA Vs SABUNI ISIYO NA DAWA
Ogea Sabuni Nzuri Zaidi Kwako; Ni Sehemu Ya Afya Yako!
Kama umewahi kuchunguza paketi za sabuni za kuogea basi utakuwa umewahi kuona maneno “Medicated Soap” na “Beauty Soap”. Unajua tofauti kati ya sabuni hizi?
“Medicated soap” ni sabuni zenye dawa. Dawa hizi husaidia kuua vijidudu kwenye ngozi yako na kukukinga dhidi ya hatari ya magonjwa na matatizo mengine yanayoweza kusababishwa na vijidudu hivyo. Hii ndio sababu ukiogea sabuni yenye dawa tatizo la harufu mbaya ya jasho linapungua au kuisha, kwa sababu harufu mbaya ya jasho huchangiwa na vijidudu jamii ya bakteria makwapani mwako na sabuni yenye dawa “Medicated Soap” husaidia kuua wadudu hao.
“Beauty Soap” haina dawa, kwa hiyo yenyewe ni kukusaidia kuondoa vumbi na uchafu mwingine tu na sio kuua vijidudu katika ngozi yako.
Mifano ya “medicated soap” ni Protex, Tetmosol, Dettol na Rungu; Mifano ya “Beauty Soap” ni Imperial, Ayu, Giv na Lux.
“Medicated soap” ni nzuri zaidi kwako kama unasumbuliwa na chunusi, muwasho, upele, harufu mbaya ya jasho nk.
Ila kama hausumbuliwi na vijidudu kwenye ngozi yako basi hata “Beauty Soap” inakufaa.
VIPI KUHUSU BEI?
Bei za sabuni hizi hazitofautiani sana, maana Rungu Medicated Soap unaweza kuipata kwa Tsh 700 na Citrus Soap ambayo ni Beauty soap unaipata kwa Tsh 700 pia; Lux Beauty Soap Tsh 2500, Protex Medicated Soap Tsh 2500 pia.
Nina imani somo hili limekusaidia kidogo kuhusu sabuni …… Endelea kufurahia kuoga kwako!
Iyo ni bei ya leja leja au ni yajumla