PATA MTAJI NA ANZISHA BIASHARA UNAYOIWAZA
Njia Ya Kwanza Ya Kupata Mtaji Na Kuanzisha Biashara Unayoiwaza
Maelfu ya watu ambao wanafurahia huduma za Afya Zaidi (AZ) Consultants wamewahi kutuambia kwamba wanatamani sana kuanzisha biashara ya Maduka ya dawa muhimu (DLDM), Famasi, Vipodozi, Zahanati na kadhalika lakini changamoto kubwa hawana mtaji. Iwe Tsh 7,000,000; Tsh 15,000,000; Tsh 25,000,000 au hata Tsh 40,000,000. Kisha sisi Afya Zaidi (AZ) Consultants tunaongea nao, kuangalia nini wanaweza kufanya na kuwashauri wafanye nini ili wapate mtaji wa kutosha kuanzisha biashara husika; mara PAAAAAP! MAMBO YANATIKI ……. Mtaji unapatikana na biashara inaanzishwa.
Hakuna siri katika hili, ila tu mambo muhimu mawili:
Kujua unataka kupata mtaji kiasi gani na lini
Kuangalia maisha yako (Mali, Mapato na Matumizi) na kuchambua njia gani zinaweza kukupa mtaji unaoutaka
Kuchagua njia inayofaa au zinazofaa kukupa mtaji na kuamua kuzitekeleza
Kuwa na imani, mstahimilivu na subira huku muda ukifanya mambo yake
Kwa mfano; Haylian Joxmetir ni Hotelier, umri miaka 24; mshahara wake ni Tsh 450,000 (Take Home) na unapitia benki; huwa anapata Tips (“Chenji baki nayo…”) kutoka kwa wateja Tsh 90,000 hadi Tsh 150,000 kwa mwezi; Wazazi wake wote wawili wapo hai na wanajiweza kiuchumi; Kodi ya chumba, mawasiliano, nauli, chakula, usafi nk kwa mwezi anatumia Tsh 280,000; Hana biashara, hafanyi dili kazini na hana chanzo kingine chochote cha mapato.
(Picha: Chumba cha hoteli anayofanyia kazi Haylian)
Haylian Joxmetir anatamani awe na biashara yake siku moja ili hata ajira yake ya hoteli ikiyumba (Kama ilivyoyumba kipindi hiki cha Corona / COVID-19) awe bado anaweza kuendelea kupata pesa kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake na kuandaa future yake. Kikwazo kikubwa kwake kwa sasa anasema mtaji. Je, afanyeje ili aweze kuanzisha biashara yake? (Afya Zaidi (AZ) Consultants tunampenda Haylian kwa sababu ni mtu mwenye akili na amewaza kitu kizuri - HONGERA KWAKE HAYLIAN!)
NJIA YA KWANZA YA KUPATA MTAJI NA KUANZISHA BIASHARA UNAYOIWAZA
Ukiweza kuanza ulipo kwa kutumia ulichonacho hiyo itakuwa njia nzuri zaidi kwako. Pata mtaji unaoutaka kwa kumega mshahara wako au kipato chako cha sasa na kuweka pembeni kama mtaji. Andika kabisa pande hilo - MTAJI WA BIASHARA XYZ. Tena usimalize matumizi yote kisha kinachobaki ndipo uweke, hapana; bali mega kwanza hicho kiasi kisha kinachobaki ndicho utumie kwa mahitaji yako. Fanya hivyo mwezi wa kwanza , wa pili, wa tatu na kadhalika hadi utakapofanikiwa kwa kufuata hatua nne hapo juu. Sio rahisi sana, inahitaji committment; ila ukiwa serious utafanikiwa pasi na shaka.
Kisha unaweza “ku-fast track” kwa kuongezea njia zingine ambazo zinafaa kwako.
Kwa mfano Haylian Joxmetir anatamani kuanza biashara ya kuuza nguo za kike (kwa mtindo wa kutembeza) kwa wanafunzi wa vyuo vilivyopo mkoani Dar es salaam na Morogoro. Ila hana mtaji, na akiulizwa angepata mtaji kiasi gani anasema tu “ningepata hata Tsh 300,000 ningeanza jamani”. Kisha unamuuliza, hiyo Tsh 300,000 mchanganuo wake ukoje - bei za jumla za nguo, utazinunua wapi, utanunuaje, utauzaje, faida kwa kila nguo moja ni kiasi gani, gharama za usafiri na matangazo kiasi gani, gharama zingine ni kiasi gani na kadhalika na kadhalika …… ILA HAPO HANA JIBU! Unajua kwa nini? Kwa sababu hakuanza hata utafiti wa biashara yake; hakujua kiasi gani haswa kinahitajika na kiasi gani anaweza kupata.
Usiwe kama Haylian Joxmetir; Usiseme tu hauna mtaji wakati hata utafiti wa mahitaji halisi ya biashara unayoiwaza haujafanya - UNAWEZA KUANDAA MTAJI PUNGUFU!
So Haylian anashauriwa kwanza afanye utafiti kiduchu ili aijue biashara anayotamani kuifanya mahitaji yake ni kama kiasi gani, cash flow ipoje, misimu yake ipoje na anaweza kupata kiasi gani; kisha ndipo aanze “kufight” ili kupata huo mtaji na kuanzisha hiyo biashara. Tuseme sasa Haylian karudi mezani, mtandaoni na sokoni kisha akapata jibu anatakiwa awe na mtaji wa Tsh 500,000 ili kuanza biashara yake ya nguo. Je, afanyeje ili kupata huo mtaji?
Now good! Anahitaji Tsh 500,000; kipato chake Tsh 540,000 - Tsh 600,000 kwa mwezi; Matumizi yake Tsh 280,000 kwa mwezi; Wazazi wake wote wawili wapo na wanajiweza …..
Huu ni mwezi wa saba; Haylian anataka ikifika tarehe 31-10-2020 awe tayari amepata mtaji na kuanza hiyo biashara mwezi wa 11. Ameshamaliza hatua ya kwanza.
Kwa maisha yake (Mapato, mali, matumizi nk) Haylian anaweza kutenga pembeni Tsh 150,000 kila mwezi na kuipa jina MTAJI WA BIASHARA YA NGUO. Anatakiwa mshahara ukitoka tu atoe hiyo Tsh 150,000 na aiweke pembeni; kisha aanze kupigia mahesabu jinsi atakavyotumia hiyo Tsh 300,000 inayobaki hadi utakapotoka mshahara ujao. So mwezi wa 8 mwishoni atakuwa na Tsh 150,000; mwezi wa tisa mwishoni itaongezeka Tsh 150,000 na atakuwa na Tsh 300,000; na mwezi wa 10 mwishoni itaongezeka Tsh 150,000 na kuwa na Tsh 450,000; Atakuwa amebakisha deni Tsh 50,000, ambayo inaweza kujazwa na Tips!
Tayari Haylian ameona njia nzuri kabisa itakayomuwezesha kupata mtaji wa Tsh 500,000 ifikapo tarehe 31-10-2020; kilichobaki ni kufuata hiyo njia, kuwa na imani, mstahimilivu, subira na kuacha muda ufanye mambo yake.
Pia Haylian anaweza kufast-track kwa kutumia Tips, kuomba kiasi kwa wazazi wake na hata kutenga zaidi ya Tsh 150,000 kila mwezi au kucheza michezo ya kupeana/kujijenga - watu watano Tsh 100,000 kila mwezi kisha aombe jina lake liwe la tatu apokee mwezi wa 9 au mwezi wa 10.
Tupo Pamoja?
Ndo hivyo tu; kwa Haylian, kwako na kwa mtu mwingine; iwe kutafuta mtaji wa Tsh 500,000; Tsh 3,000,000; Tsh 10,000,000; Tsh 50,000,000 au hata zaidi . Njia ni ile ile - Tofauti kubwa ni muda, juhudi, committment na akili tu.
(Picha: Mandhari ya nje hotelini kwa akina Haylian)
Afya Zaidi (AZ) Consultants tunawapa mwanga watu wanaotaka kuanza biashara za vipodozi, maduka ya dawa, famasi na kutoa huduma za afya - Zahanati, Hospitali, Maabara na kadhalika. Tunawasaidia kujua mahitaji halisi, ilivyo biashara yenyewe, mzunguko wa pesa, kukuza mtaji na kufungua biashara.
Tutumie meseji WhatsApp 0788179686 kama unajiandaa au umeanza ila kuna mambo yanakusumbua au unayumba kwenye biashara yako. Pia unaweza kututumia email: afyazaidi@gmail.com