Moja kati ya maswali ambayo tumeulizwa sana na fans wetu ni hili la pesa kiasi gani zinatosha kuanzishia duka la vipodozi. Vipi wewe, Umewahi kutaka kufanya biashara ya vipodozi ila ukabaki na mawazo ya kiasi cha mtaji unaotosha kufungulia duka?
Swali ambalo sisi #afyazaidiconsultants tunaulizwa na wateja wetu wengi ambao wanahitaji tuwatengenezee business plan ni "Natakiwa kuwa na mtaji angalau kiasi gani ili niweze kuanza?". Sasa Leo tunajibu kwa wote, tunakupa mbinu na wewe.
Mbinu ya kupata jibu lako ni rahisi. Hususan kama tayari una mtaji. Kama hauna mtaji basi cheki nasi pia tunashauri #njiazakupatamtaji.
Chukua peni na karatasi. Na glass ya juisi ya baridiiii na korosho au bites zingine utakazopenda.
Baada ya hapo andika mahitaji ya muhimu kwa ajili ya kuanzia duka lako au biashara yako, ambayo ni:
1. Duka au ofisi ambapo utapanga vipodozi vyako na kuuza (Aidha utajenga au utapanga)
2. Kabati la chini utakalowekea vipodozi vyako (moja, mawili nk)
3. Mashelfu ya ukutani utakayopangia vipodozi vyako (mawili, matatu nk)
4. Kibali cha duka la vipodozi kutoka Tanzania Bureau Of Standards (TBS)
5. Leseni ya biashara kutoka halmashauri
6. Cheti cha mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
7. Vipodozi na bidhaa zingine za usafi wa mwili utakazokuwa unauza dukani mwako
8. Kujitangaza - vipeperushi, mitandao ya kijamii, kupiga simu, kutuma meseji, kutembelea wadau nk
9. Kiti (viti), meza, madaftari ya kuhifadhia taarifa za biashara (records) nk
10. Umeme, maji, mawasiliano, kuhifadhia taka na vitu vingine vitakavyohitajika kulingana na eneo lako na mahitaji ya biashara yako
11. Akiba
12. Kulipa mfanyakazi na wasaidizi kama haukai mwenyewe dukani au hufanyi kazi zote mwenyewe
Sasa baada ya hapo wekea gharama ya kila kitu kuanzia hiyo namba 1 mpaka namba 10.
Mfano:
1. Duka au ofisi ambapo utapanga vipodozi vyako na kuuza (Aidha utajenga au utapanga) - Tsh 80,000 kwa mwezi; Tsh 480,000 kwa miezi 6
2. Kabati la chini utakalowekea vipodozi vyako (moja, mawili nk) - Kabati moja la chini, Tsh 300,000
3. Mashelfu ya ukutani utakayopangia vipodozi vyako (mawili, matatu nk) - Mashelfu matatu, kila moja Tsh 300,000; Jumla Tsh 900,000
4. Kibali cha duka la vipodozi kutoka Tanzania Bureau Of Standards (TBS) - Tsh 150,000
5. Leseni ya biashara kutoka halmashauri - Tsh 50,000
6. Cheti cha mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) - Tsh 200,000 kwa mwaka; Tsh 50,000 kwa robo ya kwanza ya mwaka
7. Vipodozi na bidhaa zingine za usafi wa mwili utakazokuwa unauza dukani mwako - Mzigo wa Tsh 3,000,000 unatosha kujaza duka langu
8. Kujitangaza - vipeperushi, mitandao ya kijamii, kupiga simu, kutuma meseji, kutembelea wadau nk - Tsh 300,000
9. Kiti (viti), meza, madaftari ya kuhifadhia taarifa za biashara (records) nk - Kiti cha plastic Tsh 15,000, meza ya mbao Tsh 40,000 na madaftari matatu counterbooks Tsh 6,000
10. Umeme, maji, mawasiliano, kuhifadhia taka na vitu vingine vitakavyohitajika kulingana na eneo lako na mahitaji ya biashara yako - Umeme Tsh 15,000 kwa mwezi, maji Tsh 5,000 kwa mwezi, taka Tsh 10,000 kwa mwezi, dustbin Tsh 9,000 na mawasiliano Tsh 20,000 kwa mwezi; Miezi 6 ya mwanzo Tsh 300,000
11. Akiba Tsh 1,000,000
12. Kama hautakaa mwenyewe dukani basi kulipa mfanyakazi na wasaidizi wa kazi Tsh 250,000 kwa mwezi; Tsh 750,000 kwa miezi 3
BAADA YA HAPO SASA....
Jumlisha gharama zooooote namba 1 hadi 11 kisha huo ndo mtaji unaohitajika sasa.
Kwa hiyo kwa mfano wa mahesabu hapo juu mtaji wako utakuwa Tsh 480,000 +Tsh 300,000 + Tsh 900,000 + Tsh 150,000 + Tsh 50,000 + Tsh 50,000 + Tsh 3,000,000 + Tsh 300,000 + Tsh 61,000 + Tsh 300,000 + Tsh 1,000,000 + Tsh 750,000 = Tsh 7,341,000.
Kwa hiyo mtaji wako ni Tsh 7,341,000 ambao utaweza kuendesha duka kwa miezi 3 hadi 6 bila wewe kutia pesa nyingine kutoka mfukoni mwako.
Sasa mazingira tunatofautiana sana ndio maana mtaji hauwezi kufanana. Mfano kuna mtu tayari anacho cheti cha TRA kwa hiyo hatolipia hiyo Tsh 50,000; mwingine atakaa mwenyewe dukani kwa hiyo hatolipia hiyo Tsh 750,000; mwingine fremu ni ya kwake kwa hiyo hatolipia hiyo Tsh 480,000.
Hivyo basi ili kujua utahitaji mtaji kiasi gani basi Kaa chini tafakari mahitaji ya duka lako, gharama zake na kisha jumlisha yote upate gharama ya jumla. Huo ndio mtaji unaotakiwa kuanza nao sasa.
Ukihitaji support yetu tucheki WhatsApp 0788179686 au kwa email: afyazaidi@gmail.com tukusaidie ufanikishe kuanza na kuendeleza biashara yako Bila stress.