Maduka mangapi umewahi kuona yamefunguliwa kisha yakakosa biashara na kufungwa baada ya muda tu? Hujawahi kuona biashara imefunguliwa kisha baada ya miezi 3-12 ikafa na kufungwa?
Nadhani umeona mara nyingi tu. Sasa kama na wewe uko serious unataka kuanza biashara basi jifunze kupitia makosa ya wenzako kisha epuka kufeli kama walivyofeli wao. Najua sababu za kufeli zipo nyingi kama vile usimamizi mbaya, wizi, eneo baya, mabadiliko ya sera za serikali, kulazimika kuhama eneo lako zuri, kukosa mauzo, kushindwa na ushindani, kufirisika, kufirisiwa, kesi na kadhalika. Ila hayo yote yanaongozwa na mtaji. Kama mtaji wako hautoshi basi kuyumba au kufa kabisa biashara yako kunafuatia. Labda ujikwamue au mazingira yabadilike mauzo yaongezeke, mapato yakue na ujinasue na kufeli.
Kwanza kabla hatujaendelea, unazijua kazi za mtaji?
Wiki tatu zilizopita kuna rafiki yetu mmoja aliniambia kupitia WhatsApp kwamba anataka kuanza biashara hii ya vipodozi. Nikamuuliza mtaji alionao akaniambia ana Tsh 200,000. Nikawaza na kuwazua, pesa haitoshi. Ni ndogo sana hata kwa kuanzia tu haitoshi. Fikiria kujenga au kukodi duka, kuweka makabati, kupata leseni halmashauri, kupata kibali TBS, kununua vipodozi vyenyewe na kadhalika. Unaipangilia vipi hii Tsh 200,000 itoshe yote hayo na kufanikiwa kuanzisha duka la vipodozi? Ni ngumu sana. Haiwezekani!
Sasa kama ulikuwa na mtaji wa kuanzia wa Tsh 3,000,000 na ukamudu kuanza biashara yako kwa bajeti kali utakuwa pia umeanza biashara kwa mtaji mdogo. Duka lako halitakuwa na bidhaa za kutosha, hautakuwa na mtaji wa akiba, hautaweza kujitangaza kwa kulipia, ikitokea loss kidogo tu unaenda nayo maana huna back-up wala uwezo wa kuadjust chap chap. Jaribu tu kuwaza kwa mfano ikatokea ajali ya moto na mazigo wako ukaungua pia japo kidogo, tuseme mzigo wa Tsh 1,000,000.
Kwa hiyo sio mbaya kuanza na ulichonacho, lakini usibweteke na kuamini umefika wakati mtaji uliowekeza ni mdogo. Endelea kupambana na kuongeza pesa kwenye duka lako, kuza mtaji wako hadi uwe wa kutosha. Pia kuwa na mtaji wa akiba ili ikitokea dharura uwe na back up plan.
Piga mahesabu yako vizuri, andaa plan nzuri kisha fanya utekelezaji mzuri. Epuka kukopa hususan mkopo wenye riba, utakugharimu sana endapo mambo hayataenda vizuri. Pia epuka sana kukopesha wateja wako, watakaa na mtaji wako na hata kuhama kabisa duka lako. Ni changamoto sana kwa watu wako munaojuana na kupendana, ila biashara ni biashara.
Unakumbuka jinsi ya kupangilia mtaji wako, right?
Usikosee hatua. Sometimes biashara haina huruma. Jiandae kwa mtaji wa kutosha ili uongeze uwezo wa kumudu na kufanikisha biashara yako.
Endelea kufurahia ushauri mzuri kutoka AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS. Na sisi tunaendelea kuwasaidia wajasiriamali kama wewe kuanzisha na kuendeleza biashara zao. Tunaongea nao kwa kina na kupanga mtaji unaotosha kuanzia biashara zao, kuwaandikia michanganuo ya biashara (business plans), kuwapa system ya kusimamia biashara zao, kuwasaidia kununua bidhaa zote na kuanzisha biashara zao na kadhalika.
Tunaweza kukusaidia na wewe pia. Njoo ufanikishe malengo yako!
Nawezaje kupata ushauri wa kina kutok kwenu?