KINGA DISPENSARY ISIFIRISIKE: ANZA NA WAFANYAKAZI WACHACHE, WAZURI
Unajua mambo matatu ambayo yanaweza kukufanya ushindwe ghafla kwenye biashara yako ya zahanati (dispensary)?
Unajua mambo matatu ambayo yanaweza kukufanya ushindwe ghafla kwenye biashara yako ya zahanati (dispensary)?
1. Kuchelewa kupata wateja wa kutosha kuendesha dispensary yako
2. Gharama kubwa za uendeshaji - Matumizi makubwa kwenye kulipa mishahara, kodi ya jengo, riba ya mkopo, promosheni na kadhalika
3. Kutokuwa na mtaji wa akiba wa kutosha kukusaidia kipindi chote unachokuwa unasubiri wateja wachanganye
Najua dispensary nyingi zilizokufa kwa sababu tu zilishindwa kumudu mahitaji na matumizi. Wafanyakazi wakaondoka kwa sababu ya kucheleweshewa mishahara yao, wateja wakapungua kwa sababu ya huduma mbovu au kukosa huduma kabisa, dispensary ikawa inajiendesha kwa hasara na taratibu ikafa.
Ukija kwetu kutaka ushauri cha kwanza tunaangalia tatizo ni nini na chanzo ni nini. Kisha tunaangalia ufumbuzi wa tatizo hilo ni nini, nini hakipo (gap) na mambo gani yafanyike ili kulitatua hilo tatizo.
So kwa kesi kama hiyo tunaweza kuangalia namna ya kuongeza mtaji, kuboresha huduma, kukidhi mahitaji ya wafanyakazi, kufanya matangazo na kudhibiti matumizi ili faida ipatikane na ibaki ya kutosha.
Unaweza kufanikiwa kwa urahisi zaidi endapo utajikita kuanza katika huduma zenye wateja wengi tayari na kuanza na idadi ya wafanyakazi muhimu tu kwanza. Kisha kuongeza huduma na wahudumu pole pole kadiri unavyozidi kupata biashara.
Ndo hivyo wenzako wanavyofanikiwa katika biashara. Mara zote hakikisha matumizi yako hayazidi mapato. Na kazi yako kubwa ni kukidhi mahitaji ya wateja wako na kutengeneza faida.
Fanya biashara vizuri. Fuata njia za mafanikio.
- AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS.