KARIBU UWEKEZE KATIKA BIASHARA
Kama una mtaji kiasi na unataka kuanza sasa basi tumia fursa hii ....
Hi! Unaonaje siku zinavyoenda? Zinakimbia sana!
Yaani juzi tu hapa tulikuwa tunasherehekea mwaka mpya, ila sasa unastuka tayari ni mwezi wa tano. Muda unakimbia sana …..
Sasa just imagine ungewekeza Tsh 5,000,000 katika biashara ya famasi, duka la vipodozi, vifaa vya maabara, hospitali na kadhalika ambapo ungeambiwa kwamba utapata faida ya 10% kwa mwezi. Ina maana faida ya Tsh 500,000 kila mwezi. Mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu na wanne tayari ungekuwa na faida ya Tsh 2,000,000 huku mtaji wako ukiwa pale pale. Tsh 5,000,000 + Tsh 2,000,000 = Tsh 7,000,000; ndio pesa ambayo ungekuwa nayo kwa sasa. Ungekuwa na faida. Mtaji wako ungekuwa umekua!
Sasa miezi minne imeenda tayari. Ila kuna miezi mingi inakuja, na fursa nyingi zinakuja. Leo tuhame kidogo kutoka elimu na ushauri na tuhamie kwenye ufanyaji kwa vitendo wa yale mambo ambayo tumekuwa tukielimishana na kushauriana.
Kama AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS kazi yetu kubwa sana ni kujengea uwezo wafanyabiashara na watu wanaotaka kufanya biashara za huduma za afya, dawa, vipodozi, vifaa vya maabara nk. Kukuwezesha wewe upate data kamili, connections, makadirio ya mtaji, mpangilio wa matumizi ya mtaji, watu wa kushirikiana nao, kuanzisha na kusajili biashara yako, kuwekeza kwenye biashara za watu wengine na kadhalika. Ili mradi tu lengo lako litimie - uanze biashara yako, ukuze mtaji wako, utengeneze faida na kadhalika.
Tuanze sasa …..
Lengo lako kubwa ni lipi?
Vitu gani vinatakiwa ili kutimiza lengo lako?
Vitu gani tayari unavyo na vitu gani bado hauna?
Upo tayari kufanya nini au kutoa nini ili kutimiza lengo lako?
Tuna nafasi kadhaa kwa watu wetu mbalimbali. Angalia nafasi ipi itakufaa kisha uje tuanze kufanya kazi.
Kama tayari una mtaji wa Tsh 5,000,000 na kuendelea unaweza kuanzisha biashara yako kama mtaji unatosha. Mfano kama tayari una Tsh 20,000,000 basi unaweza kuanzisha Famasi yako; kama una Tsh 5,000,000 basi unaweza kuanzisha duka lako la vipodozi; kama una Tsh 40,000,000 basi unaweza kuanzisha zahanati (dispensary) yako.
Kama mtaji wako hautoshi basi unaweza kuungana na wenzako wenye mtaji kiasi kidogo kama wewe kisha mkatimiza mtaji unaotakiwa na kuanzisha biashara ya pamoja, partnership. Kwa mfano wewe una Tsh 5,000,000 na watu wengine watatu wana Tsh 5,000,000 kila mmoja; jumla ni Tsh 20,000,000 na hivyo kuwa mtaji wa kutosha kuanzisha famasi yenu ya ushirika.
Pia kama mtaji wako hautoshi basi unaweza kuukuza kwa kuwekeza kwenye biashara inayojiendesha vizuri tayari lakini ina mahitaji kiasi ya mtaji ili ipige hatua kubwa au ya haraka. Mfano Tsh 5,000,000 yako unaiweka kwenye biashara ya famasi au duka la vifaa vya maabara au zahanati ya mtu/kampuni kwa makubaliano ya mgao wa faida wa 10% kila mwezi au kila deal likikamilika. Ina maana baada ya mwezi mmoja utatengeneza faida ya Tsh 500,000; miezi miwili Tsh 1,000,000; miezi 6 Tsh 3,000,000; na mwaka mmoja Tsh 6,000,000 huku mtaji wako ukiwa pale pale. Utaamua mwenyewe lini unachukua faida yako na ule mtaji wako - labda mfano jumla ikifika Tsh 20,000,000 ili ukaanzishe famasi yako
So jiangalie nafasi yako kwa sasa na nini unaweza kuanza nacho. AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS tutakujengea uwezo na kukusaidia kutimiza malengo yako.
Tayari tuna biashara za watu ambazo zinaendelea vizuri na wapo tayari kupokea mtu ambaye atawekeza fedha na wagawane faida kila mwezi au deal likikamilika. Kuna supplier wa vifaa vya maabara, supplier wa vifaa vya hospitali, supplier wa dawa/famasi ya jumla, famasi za rejareja na kadhalika. Na pia tuna watu wenye mtaji kiasi ambao wanatafuta watu wengine wenye mtaji kiasi ili waunganishe nguvu na kuanzisha biashara kwa pamoja.
Tunatafuta watu ambao wako interested kuanza biashara sasa kisha tuwaunganishe na kuwajengea uwezo waanze kwa mafanikio.
Kama upo interested tujulishe ili tukuunganishe na kusaidiana kwa pamoja kutimiza malengo yetu.
AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS
0788179686 | afyazaidi@gmail.com