KABLA YA KUNUNUA FAMASI KUTOKA KWA MTU ZINGATIA HAYA ....
Ni changamoto gani zinamfanya aiuze? Je, wewe utaweza kuzimudu hizo changamoto na kufanikiwa kibiashara?
Famasi ni moja kati ya biashara nzuri sana. Ukiona mtu anauza famasi yake basi jua ana changamoto kadha wa kadha zinazomlazimu afanya hivyo. Aidha changamoto za usimamizi, migogoro miongoni mwa wamiliki, kuhama mkoa, kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa kwa haraka, kufilisika, mwenendo mbaya wa biashara, kuhitaji kubadili biashara na kadhalika.
Kabla ya kununua famasi inayouzwa basi fanya utafiti kidogo ujue changamoto haswa ni nini - sababu binafsi za mmiliki/wamiliki, migogoro au eneo halina biashara?
Ukiwa na uhakika kwamba unazielewa na kuzimudu hizo changamoto basi sawa, nunua; ila kama hauna uhakika kwamba unazielewa na unazimudu hizo changamoto basi subiri kwanza.
Usipoteze Tsh 20,000,000 - Tsh 30,000,000 kisha uhangaike kuanza kuzitafuta, ukizikosa utajilaumu sana. Kuna baadhi ya famasi mmiliki wake amejitahidi kila linalowezekana lakini wapi, hakuna biashara; na kuna baadhi ya famasi ni vile tu mmiliki wake hakuwa na uwezo ndio maana ziliyumba na kuuzwa.
Fanya utafiti. Pata ushauri.
#hospitali