JINSI UNAVYOWEZA KUPATA PESA KUPITIA VIPODOZI
Unaweza kuanza na mtaji mdogo na kufanikiwa kupata faida nzuri. Pita njia nzuri ....
Miaka ya 2010-2012 wakati bado nipo chuo kikuu niliwahi kuona marafiki zangu wengi wakijiunga na biashara za mtandao (network marketing) kama vile Oriflame, Forever Living, GNLD (Kwa sasa Neolife) na kadhalika. Lengo lao kubwa lilikuwa ni kutafuta pesa na kujenga mazingira ya kuwa na biashara wakimaliza chuo. Kujiunga huko ilikuwa ni kupitia mdhamini (sponsor) na kwa kununua bidhaa za kuanzia ambazo zilikuwa kati ya Tsh 23,000 hadi Tsh 450,000 kisha uende ukatumie au ukauze bidhaa hizo. Bidhaa zenyewe nyingi zilikuwa ni vipodozi na virutubisho (nutritional supplements).
Kwa wengi haikuwa rahisi. Hatimaye wachache sana walifaulu kidogo, ila wengine walio wengi walikata tamaa wakaacha na wengine wakaendelea ila kwa kujikongoja kwa tabu sana huku wakitegemea zaidi kuunganisha watu wapya ili wao wapate kamisheni kuliko wao kuuza hizo bidhaa za hayo makampuni. Mwingine ilimchukua zaidi ya mwezi kupata mteja wa zile bidhaa za Tsh 450,000; na wengine waliishia kuziweka famasi ili akitokea mteja ziuzwe tu hapo angalau mtaji urudi.
Unajua kwa nini wengi walifeli? Baadhi ya sababu za wao kufeni ni hizi hapa:
1. Wengi wao walikuwa hawana upeo mzuri wa biashara ya network marketing na walijiunga kwa sababu tu walijulishwa kwamba huko mambo ni mazuri na watu wanafanikiwa sana kupata pesa nyingi, magari ya kifahari, safari nyingi kwenda nje ya nchi, kulala hoteli za kifahari na kadhalika
2. Wengi wao hawakujua kazi kubwa iliyopo mbele yao - kuuza bidhaa za kuongeza wauzaji wengine wa bidhaa za kampuni hivyo walifanya kazi hiyo kivivu muda ambao wamemaliza madarasa na siku za week end na sikukuu.
3. Wengi wao hawakuwa na watu wenye mawasiliano nao na wenye matatizo yanayohitaji bidhaa hizo. Hatimaye walikuwa wanatangaza kwa watu wachache na kuuza kidogo sana au kushindwa kuuza kabisa.
Kwa hiyo wengi walifeli kwa sababu walishindwa kuuza bidhaa za kutosha na kuongeza wauzaji wa bidhaa hizo.
Sasa tukija kwenye biashara ya vipodozi kuna maneno nayasikia mtaani kwamba biashara ya vipodozi ina hela sana. Yaani ukiwekeza million mbili (Tsh 2,000,000) zako tu baada ya muda unaanza kutengeneza pesa nyingi. Nikisikia hivyo nakumbuka zile story za Oriflame, Forever Living, GNLD nk na kujiuliza: hivi hawa watu wamewahi kufanya biashara hii au wamesikia tu?
Ukweli ni kwamba biashara ya vipodozi ni biashara kama biashara zingine – Unavuna ulichowekeza na kuuza. Kwa hiyo vitu muhimu ni viwili:
1. Kiasi ulichowekeza
2. Mauzo yako
Jinsi unavyoweza kupata pesa
Huwa nawafundisha watu na kuwashauri vizuri tangu kuandaa mpango wa biashara (business plan), kutafuta mtaji kidogokidogo, kutafuta eneo la kuweka duka (location), kusajili biashara (na kupata leseni halmashauri/manispaa, TIN ya TRA nk), kufungua duka hadi kuanza kuuza na kuzoea biashara hii kiasi cha kuweza kujitegemea bila msaada wangu wa karibu tena.
Kiuhalisia biashara ya vipodozi ina faida kama biashara zingine, ila tu kizuri zaidi ni kwamba vipodozi vinatumiwa kila siku havina msimu na watumiaji wake ni wengi sana kwa hiyo soko lake ni kubwa.
Jinsi ya kupata pesa ni kama biashara zingine tu, nunua vipodozi kwa bei ndogo (bei ya jumla) na kasha uza kwa bei kubwa kuliko ile uliyonunulia (bei ya rejareja). Kwa mfano nunua losheni ya nivea kopo kubwa la ujazo wa 400mls kwa Tsh 8,500 na kasha wewe uza kwa Tsh 12,000. Ukiuza unapata pesa Tsh 3,500.
# Nunua perfume kwa Tsh 18,000 na kisha wewe uza kwa Tsh 25,000. Ukiuza unapata pesa Tsh 7,000.
# Nunua sabuni kwa Tsh 2,000 na kisha wewe uza kwa Tsh 2,500. Ukiuza unapata pesa Tsh 500.
# Nunua body spray kwa Tsh 3,500 na kisha wewe uza kwa Tsh 5,000. Ukiuza unapata pesa Tsh 1,500.
Na wateja wapo. Tena wengi sana; cha muhimu ni kuweka biashara walipo au wanapopita, na kuweka vitu wanavyohitaji na kuuza kwa bei wanayoimudu.
Jinsi ya kupata pesa nyingi
Jinsi ya kupata pesa nyingi ni kuweka biashara yako mahali penye mzunguko mkubwa wa biashara au kutengeneza mzunguko mkubwa wa biashara. Ni rahisi tu kama hivyo, yaani uwe na wateja wengi au uwe na wateja wakubwa wanaonunua bidhaa nyingi.
Ukiwa na mzunguko wa kuuza pafyumu 5 kila siku na kufanya kazi jumatatu hadi jumamosi (Siku 26 kwa mwezi) ina maana kwa mwezi utauza pafyumu 130 na kupata faida ya Tsh 910,000. Faida ya Tsh 910,000 kwa mwezi, na hiyo ni kutoka kwenye pafyumu tu. Hapo bado losheni, sabuni, body spray, mawigi na kadhalika.
Kwa mfano ukinunua na kuuza:
o Ukinunua pafyumu 130 kwa Tsh 18,000 kila moja na kuziuza kwa Tsh 25,000 kila moja utapata faida ya Tsh 7,000 x 130 = Tsh 910,000
o Ukinunua losheni 130 kwa Tsh 8,500 kila moja na kuziuza kwa Tsh 12,000 kila moja utapata faida ya Tsh 3,500 x 130 = Tsh 455,000
o Ukinunua sabuni 130 kwa Tsh 2,000 kila moja na kuziuza kwa Tsh 2,500 kila moja utapata faida ya Tsh 500 x 130 = Tsh 65,000
o Ukinunua body spray 130 kwa Tsh 3,500 kila moja na kuziuza kwa Tsh 5,000 kila moja utapata faida ya Tsh 1,500 x 130 = Tsh 195,000
Kwa bidhaa hizo nne tu utapata pesa kiasi cha Tsh 910,000 + Tsh 455,000 + Tsh 65,000 + Tsh 195,000 = Tsh 1,625,000.
Yaani utapata faida ghafi (gross profit) ya Tsh 1,625,000 kwa mwezi kwa bidhaa hizo nne tu; bado bidhaa zingine. Kwa ujumla sio mbaya, kikubwa uwe na mzunguko mzuri wa wateja na uwe na uwezo mzuri wa kuuza bidhaa zako kwa wateja.
Kwa hiyo mimi nakuambia tu kwamba pesa ipo; ila kiasi cha pesa kinategemea na maandalizi yako na juhudi zako. Unaweza ukapata hasara, ukatengeneza pesa kidogo au ukatengeneza pesa nyingi.
Usianze mwenyewe na kupoteapotea au kupoteza pesa zako, fanya biashara kitaalam uwe na nafasi kubwa ya kufanikiwa.
Bado kuna mambo mengi ya kujifunza na kujiandaa kama vile kiasi gani kinafaa kuanzia biashara hii, njia za kutumia ili kutimiza mtaji, mahali panapofaa kuweka biashara, kusajili kukodi eneo/duka, kusajili biashara yako, kununua mzigo (vipodozi), kupanga bei, kutangaza biashara, kuuza kwa wateja, kukuza mtaji, kuvuna faida, changamoto zilizopo na kuzikabili na mambo mengine mengi. Ukiijua vizuri biashara ya vipodozi na kuifanya vizuri basi jua tu kwamba faida ipo na utafanikiwa kuipata.
Umeiona biashara ya vipodozi? Vipi sasa, unataka kuifanya au basi? Maswali gani bado unajiuliza?
Niambie nami nitakuambia. WhatsApp 0788179686.
Afya Zaidi (AZ) Consultants
0719326693 | 0743422883
Hakika nmekulew vizur mkuu
mafunzo yako nimazuri sana