Umewahi kutumia bidhaa ambayo umeizoea ila ukaiona kama iko tofauti kidogo?
Labda ladha, rangi, harufu, uzito, muonekano, bei, maandishi na kadhalika. Hiyo ndo namna rahisi zaidi ya kuanza kuhisi kama bidhaa uliyonunua au kutumia ina walakini.
Sasa ili kuepuka bidhaa feki fanya hivi:
Usinunue bidhaa za mkononi au zinazopangwa chini. Zingatia supply chain rasmi ya bidhaa husika kutoka kiwandani hadi kwako mtumiaji
Ukiona bidhaa ina tofauti kidogo na ile original uliyoizoea basi iache, inaweza kuwa na walakini. Iwe ni ladha, rangi, harufu, uzito, muonekano, bei, maandishi na kadhalika. Hushangai bidhaa nyingi feki za kichina zinakosewa sana kiingereza chake?
Scan QR Code au Bar code ya bidhaa husika ili kuverify uhalisia wake
Basi ndo hivyo. Itakusaidia sana. Sisi AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS tupo kwa ajili ya kukusaidia wewe kupata mahitaji yako na kufurahia matokeo mazuri.