Hi! Kuna hype umewahi kuisoma mahali au kuisikia kwenye pitapita zako za biashara kwamba biashara ya famasi inalipa sana. Na kwa kuwa kila mtu anatamani "biashara inayolipa kwa uhakika" basi mtego huu unaweza ukakunasa. Ngoja tucheki mawili matatu kisha uwe na muono mpana zaidi ili uweze kutafakari na kuamua kwa usahihi.
SWALI 1: "Vipi biashara ya famasi rafiki yangu, INALIPA" ?
JIBU: Yeah, biashara ya famasi inalipa; ila.... vigezo na masharti kuazingatiwa. So far kuna wenye famasi ambao famasi zao zinawalipa, kuna ambao haziwalipi na kuna ambao wapo katikati - hawajaanza kupata faida lakini pia hawapati hasara.
Gharama za uendeshaji wa famasi ni kubwa. Sio chini ya Tsh 2,000,000 kwa mwezi. Kwa msingi huo ni lazima uwe na mauzo ya kutosha kukupa faida ghafi (gross profit) ya angalau Tsh 2,000,000 kwa mwezi ili uweze kumudu gharama za uendeshaji hapo juu.
SWALI 2: "Kama inalipa kwa nini wengine wanafunga au wanauza famasi zao"?
JIBU: Sababu kubwa ni mmiliki/wamiliki kushindwa katika uendeshaji wa famasi husika- Aidha bado haijafikia hatua ya kujitegemea na wanatoa pesa mfukoni kila siku ili kuisapoti au wanahama mkoa hivyo kushindwa kuwa karibu au wamefilisika kifedha au wamehitilafiana na kukubaliana wauze ili kila mtu aendelee na mambo yake mengine. Na wengine wanauza famasi ili kuboost mtaji wao wafanye biashara nyingine ambayo wana imani nayo zaidi - mfano biashara ya magari, chuo nk. Unauza famasi Tsh 25,000,000; Shamba Tsh 20,000,000; Nyumba Tsh 40,000,000; unachukua mkopo benki Tsh 100,000,000 na kadhalika hadi upate Tsh 200,000,000 kwa ajili ya kujilipua kwenye biashara ya magari; Eennhhee maana faida yake ni kubwa zaidi na magari hayaozi bhana!
Ukitaka kununua famasi unaweza kuuliza kwa nini yeye anaiuza na kumuomba akuweke wazi changamoto ambazo zipo ili wewe ujipange na uingie vizuri. Kufeli kwa mmiliki wa awali sio kufeli kwa mmiliki mpya; na kama unazo pia au hujatatua changamoto zilizomfanya mwenzako auze hiyo famasi basi na wewe unaweza kufeli pia.
SWALI 3: "Natamani kufungua famasi; niandae mtaji kiasi gani"?
JIBU: Andaa kiasi kuanzia Tsh 20,000,000; ukiwa na mtaji mkubwa zaidi utaweza kufungua famasi kwenye "Premium Location", kuwa na bidhaa za kutosheleza sehemu kubwa ya wateja wako na kuweza kuendelea na maisha yako bila kutegemea mauzo ya famasi ili upate kula nyumbani, ulipe ada za watoto, utie mafuta gari yako na kadhalika. Uliona wapi mzazi anaanza kumtegemea mtoto ambaye ndo kwanza amemzaa? Kwa maeneo yaliyochangamka na kuwa na "potential" ya biashara kodi ya fremu (minimum) inaweza kuwa Tsh 500,000 na kuendelea, hivyo ukilipa ya miezi 6 (minimum) tayari 2,400,000 zimeenda; humo ndani utaweza shelves na milango ya aluminium na vioo - si ajabu Tsh 4,000,000 kuishia hapo. Utanunua friji, utafanya partition, utaweka AC, viti, meza nk - Tsh 1,000,000 imeenda tena; Then utalipia ukaguzi, usajili, leseni nk serikalini kupitia Pharmacy Council, Halmashauri ya mji au Manispaa, TRA na kadhalika; Sio chini ya Tsh 800,000 huo mchakato. Baada ya hapo nunua dawa na bidhaa zingine za kuuza Famasi kwako, Minimum Tsh 10,000,000.
Then hamini nakwambia wateja ni kama wana makusudi, wataanza kuja na kutaka dawa ambazo wewe kwa sasa hukuanza nazo. Huwezi kushindana na wateja - utafunga duka; chukua pesa nenda kanunue dawa zao wawekee.
NB: Hutakiwi kumaliza mtaji wako wote, lazima ubaki na kiasi cha pesa kuweza kumudu mahitaji mengine ya dawa na mambo mengine ambayo yatajitokeza mbele ya safari.
So kuna watu wameanzisha famasi kwa Tsh 15,000,000; wengine Tsh 25,000,000; wengine Tsh 35,000,000; na wengine Tsh 50,000,000; HAPO TUNAZUNGUMZIA FAMASI ZA REJAREJA!
SWALI 4: "Faida ya famasi ipoje?"
JIBU: Chanzo kikubwa cha faida kwenye famasi ni ile itokanayo na mauzo ya dawa - wewe unanunua kwa jumla kisha unauza kwa rejareja; kwa mfano unanunua SONADERM Tsh 2,900 kisha wewe unauza kwa Tsh 3,500; faida yako Tsh 600. Unanunua Bio Oil kwa Tsh 10,900 kisha wewe unaiuza kwa Tsh 14,000; faida yako Tsh 3,100.
Pia utaweza kuuza vipodozi, bidhaa za usafi wa mwili, lishe, vifaa vya kusaidia wagonjwa kusikia, kutembea na kadhalika.
Kadiri unavyouza zaidi ndivyo unavyopata faida zaidi. Utapata faida kiasi gani inategemea na upangaji wako wa bei na mauzo utakayoyafanya. Najua kuna famasi ambazo zinauza SONDAERM Tsh 4,000 hadi Tsh 5,000 hivyo faida yao kuwa Tsh 1,100 hadi Tsh 2,100. ILA KAMA UPO BUZA, MBAGALA, TANDALE, GONGO LA MBOTO, GOBA NK BASI USIWAIGE WAO! Wenzako wako Oysterbay mteja anakuja amepaki RANGE ROVER VELAR hapo nje, huko BUNJU......
SWALI 5: "Nikitaka kuwin katika biashara ya famasi nifanyeje"?
JIBU: Famasi ni biashara kama biashara zingine, isipokuwa tu hii ni sensitive na inatazamwa sana na serikali. Fungua duka lako mahali penye mahitaji ya kutosha (good location - karibu na hospitali? kwenye movement kubwa ya watu? kwenye makazi ya watu wengi? kwenye njia ya vibosile?), shinda ushindani, uza bei kulingana na uwezo wa wateja wako walio wengi, weka bidhaa ambazo zinatatua matatizo ya wagonjwa wako, usiitegemee famasi yako kabla haijakomaa, kuwa na akiba ya mtaji wa kuboost famasi yako ikilegalega, zingatia sheria, kidhi mahitaji ya wateja wako wengi, nunua dawa kwa bei ya chini, lipa madeni kwa wakati, kuwa na network kubwa, kuwa na wauzaji wazalendo kwako, simamia duka lako kila siku, shirikiana vizuri na wafanyabiashara wenzako, kubali try and error, piga vizuri mahesabu ya biashara yako kila siku/wiki, dhibiti wizi dukani, kuwa makini na dawa zinazokaribia kuexpire, usiuze hakuna na kadhalika.
USIENDE KWA MGANGA, Utaibiwa bure tu!
So kwa ujumla biashara ya famasi ni kweli inalipa. Inalipa malaki hadi mamilioni, vigezo na masharti kuzingatiwa. Kadiri unavyokuwa na mtaji mkubwa, FOCUS, menejimenti nzuri, customer care nzuri, kuweka bidhaa muafaka kwa wateja wako na kutokuwa na matatizo na baraza la famasi, halmashauri ya mji/manispaa, TRA, wafanyakazi wako, wanaokuuzia mzigo nk basi nafasi yako ya kufanikiwa inakuwa nzuri sana.
Kila la kheri katika kuendelea kuangalia kwako!
Nimefurahi sana kuweza kupata muda na kushare na wewe mambo hayo matano. Nikipata muda siku nyingine tutashare mambo mengine maana naamini kuna yatakayokusaidia na kukuwezesha kuanzisha au kuboresha biashara - aidha ya famasi au vipodozi.
Ukiwa na mahitaji zaidi au umekwama unahitaji ushauri wa kitaalam basi karibu sana. Tuwasiliane kwa contacts zifuatazo:
@ AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS | 2020
afyazaidi@gmail.com | 0719326693 | 0743422883
Thanks for your advice
This article is so helpful to me. I'll contact you for more professional advice